WAJUMBE wa Kamati ndogo ya Mabadiliko ya Katiba ya Yanga walioteuliwa juzi, jana walishiriki semina ya kuwajengea ufahamu juu ya ripoti ya mabadiliko katika hatua hii ya awali iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Ikumbukwe juzi, Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk Mshindo Msolla aliwateua wanachama wanane kuunda Kamati Ndogo ya Mabadiliko, ambao ni (Mwenyekiti) Wakili Raymond Wawa na Wajumbe; Wakili Sam Mapande, Wakili Audats Kahendagile, Wakili Imani Madega, Wakili Mark Anthony, Mohammed Msumi, Pastory Kyombya na Deborah Mkemwa.
0 comments:
Post a Comment