
KIKOSI cha Simba SC kimerejea leo Dar es Salaam kutoka Zimbabwe ambako Jumatano walichapwa 1-0 na wenyeji, FC Platinums jana Uwanja wa Taifa wa Harare katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa.

Simba SC inaelekeza nguvu zake katika mchezo wa marudiano Januari 6 Uwanja wa Mkapa – ikihitaji ushindi wa 2-0 ili kuingia hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment