MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC ya Dar es Salaam wamepangwa Kundi B katika Kombe la Mapinduzi pamoja na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar ya Morogoro na Chipukizi FC ya Pemba.
Vigogo Yanga SC ya Dar es Salaam pia wamepangwa Kundi A pamoja na Namungo FC ya Lindi na Jamhuri FC ya Pemba pia.
Kundi C linazikutanisha Azam FC ya Dar es Salaam na vigogo wa visiwani, Malindi FC na Mlandege FC ambao ndio mabingwa wa Zanzibar.
Michuano hiyo itaanza Januari 5, mwakani Yanga SC ikimenyana na Jamhuri usiku baada ya Mtibwa Sugar kucheza na Chipukizi jioni.

RATIBA KAMILI KOMBE LA MAPINDUZI
Januari 5, 2021
Yanga SC v Jamhuri
Mtibwa Sugar v Chipukizi
Januari 6, 2021
Malindi FC v Mlandege
Januari 7, 2021
Simba SC v Chipukizi
Januari 8, 2021
Azam FC v Mlandege FC
Yanga SC v Namungo FC
Januari 9, 2021
Jamhuri FC v Namungo FC
Simba SC v Mtibwa sugar
Januari 10, 2021
Azam FC v Malindi FC
ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
Mwaka Bingwa Mshindi wa Pili
2007 Yanga SC Mtibwa Sugar
2008 Simba SC Mtibwa Sugar
2009 Miembeni KMKM
2010 Mtibwa Sugar Ocean View
2011 Simba SC Yanga SC
2012 Azam FC Simba SC
2013 Azam FC Tusker FC
2014 KCCA Simba SC
2015 Simba SC Mtibwa Sugar
2016 URA Mtibwa Sugar
2017 Azam FC Simba SC
2018 Azam FC URA FC
2019 Azam FC Simba SC 2-1
2020 Mtibwa Sugar Simba SC 1-0
0 comments:
Post a Comment