MSHAMBULIAJI Marcus Rashford jana amefunga mabao mawili dakika ya 26 na 51, Manchester United ikitoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Bramall Lane.
Bao lingine la Manchester United lilifungwa na Anthony Martial dakika ya 33, wakati mabao ya Sheffield United yalifungwa na David McGoldrick dakika ya tano na 87.
Kwa ushindi huo, kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kinafikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi 12 na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya 10, ikizidiwa pointi tano na vinara, Liverpool ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment