Mshambuliaji Mbrazil Neymar akipongezwa na wenzake baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa 5-1 wa Paris Saint-Germain dhidi ya Istanbul Basaksehir kwenye mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Parc des Princes, Jijini Paris.
Neymar alifunga mabao yake dakika za 21, 38 na 50, wakati mabao mengine ya PSG yamefungwa na Kyllian Mbappe kwa penalti dakika ya 42 na 62 na la Istanbul Basaksehir lilifungwa na Mehmet Topal dakika ya 57.
Mechi hiyo ilivunjika juzi baada ya wachezaji wa Istanbul Basaksehir kugoma wakimlalamikia refa wa akiba, Mromania Sebastian Coltescu kumtolea kauli za kibaguzi kocha wao Msaidizi, Pierre Webo
PSG imemaliza na pointi 12 sawa na kuongoza Kundi H ikiizidi kwa wastani wa mabao tu RB Leipzig na zote zinakwenda Hatua ya 16 Bora PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment