
Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva wa Wydad Athletics akijaribu kupiga mpira mbele ya beki wa Olympic Safi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro jana Uwanja wa El Massira mjini Safi. Olympic Safi ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Thierry Kassi dakika ya 26 na Mehdi Zaya dakika ya 76, wakati la Wydad lilifungwa na Muaid Ellafi dakika ya 55.

0 comments:
Post a Comment