TIMU ya Manchester United leo imeibuka na ushindi wa 6-2 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Scott McTominay dakika ya pili na ya tatu, Bruno Fernandes dakikaya 20 na la penalti dakika ya 70, Victor Lindelof dakika ya 37 na Daniel James dakika ya 66, wakati ya Leeds United yamefungwa na Liam Cooper dakika ya 42 na Stuart Dallas dakika ya 73.
Sasa Manchester United inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 13 na kusogea nafasi ya tatu, wakizidiwa pointi moja na 2 Leicester City wanaoshika nafasi ya pili nyuma ya Liverpool wanaoongoza kwa pointi zao 31, ingawa wote wamecheza mechi moja moja zaidi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment