Manchester United imetoa sare ya 2-2 na wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa King Power.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 23 na Bruno Fernandes dakika ya 79, wakati ya Leicester City yamefungwa na Harvey Barnes dakika ya 31 na Axel Tuanzebe aliyejifunga dakika ya 85 baada ya kubabatizwa na mpira uliopigwa wa Jamie Vardy.
Sasa Manchester United inafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 14, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikiendelea kuzidiwa pointi moja na Leicester iliyocheza mechi moja zaidi, wote wakiwa nyuma ya Liverpool inayoongoza kwa pointi zake 31 za mechi 14 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment