Manchester City imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Arsenal jana Uwanja wa Emirates, London.
Mabao ya Manchester City yalifungwa na Gabriel Jesus dakika ya tatu, Riyard Mahrez dakika ya 54, Phil Foden dakika ya 59 na Aymeric Laporte dakika ya 73, wakati la Arsenal lilifungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 31.
Mechi nyingine ya Robo Fainali jana Carabao Cup, Brentford iliichaa Newcastle United 1-0 Uwanja wa Brentford Community, bao pekee la Joshua Dasilva dakika ya 66.
Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi mbili, Stoke City na Tottenham Hotspur Saa 2:30 Uwanja wa bet365 na Everton na Manchester United Saa 5:00 usiku Uwanja wa Goodison Park PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment