MBRAZIL Roberto Firmino akishangilia baada ya kuifungia Liverpool mabao mawili dakika za 44 na 68 katika ushindi wa 7-0 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Selhurst Park, London.
Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Takumi Minamino dakika ya tatu, Sadio Mane dakika ya 35, Jordan Henderson dakika ya 52 na Mohamed Salah dakika ya 81 na 84 na kwa ushindi huo mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 14 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi sita zaidi ya Tottenham Hotspur ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment