Gerard Houllier amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 73 wiki tatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo Jijini Paris PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KOCHA wa zamani wa Liverpool na Aston Villa, Gerard Houllier amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 73 wiki tatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo Jijini Paris.
Mfaransa huyo ambaye pia amefundisha Paris Saint-Germain na Lyon za kwao, amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya Kiafya kwa muda, tatizo lake kubwa likiwa ni moyo na shinikizo la damu - lakini sababu ya kifo chake bado haijulikani.
Houllier, aliyeiongoza Liverpool kutwaa mataji matatu mwaka 2001, anapewa heshima kubwa mno na wachezaji aliowafundisha enzi hizo wakisema ni kocha wa kiwango cha juu kitaaluma, mwenye haiba halisi ya kiume na asiyepoenda kujikweza.
Kwa pamoja kituo cha Radio cha RMC na gazeti la L'Equipe, vyombo vya Habari vya Ufaransa vimeripoti kwamba Houllier amefariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo Jijini Paris. Kwa mujibu wa mwandishi wa jarida la L'Equipe, Vincent Duluc, Houllier alikwenda kufanyiwa upasuaji huo wik tatu zilizopita na alitolewa hospitali kurejeshwa nyumbani Jumapili.
Aliripotiwa kutuma ujumbe wa maandishi kwa simu mwishoni mwa wiki ukisema: "Nahangaika, lakini nitaondoka katika hali hii,".
0 comments:
Post a Comment