Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MABINGWA watetezi, Simba SC leo wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya kocha Mbelgiji, Sven-Ludwig Vandenbroeck ifikishe pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, sasa ikizidiwa pointi tano na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.
Haukuwa ushindi mwepesi kwa Wekundu wa Msimbazi hivi leo, kwani walilazimika kusubiri hadi dakika ya 76 kupata bao hilo, mfungaji akiwa ni mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere.

Kagere aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nahodha, mshambuliaji John Bocco alifunga bao hilo kwa penalti kufuatia refa Heri Sasii wa Dar es Salaam kusema mchezaji mmoja wa KMC aliunawa mpira uliopigwa na beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Wachezaji wa KMC wakiongozwa na Nahodha wao, Juma Kaseja walimfuata refa kupinga maamuzi yake, lakini mwishowe wakakubali adhabu hiyo na ‘MK 14’ Kagere kama kwaida yake akafunga.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula/Beno Kakolanya dk46, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Francis Kahata, Muzamil Yassin/Chris Mugalu dk62, John Bocco/Meddie Kagere dk46, Clatous Chama na Luis Miquissone.
KMC; Juma Kaseja, Israel Mwenda, Ally Ramadhan, Andrew Vincent ‘Dante’, Lusajo Mwaikenda, Jean Baptiste Mugiraneza, Kenny Ally, Mohammed Samatta/Kelvin Kijili dk62, Relliant Lusajo/Paul Peter dk68, Emmanuel Mvuyekure na Hassan Kabunda/Massoud Abdallah ‘Cabaye’ dk75.
0 comments:
Post a Comment