SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limemfungia miezi sita kiungo wa Namungo FC na kuitoza faini ya dola za Kimarekani 127, wastani wa Shilingi Milioni 290 klabu yake ya zamani, Simba SC.
Hatua hiyo malalamiko ya klabu ya zamani wa mchezaji huyo, Pharco ya Misri ambao wamedai mchezaji huyo hakufuata taratibu za kuondoka.
Kaimu Mwenyekiti wa Simba SC, Mwina Kadugua amesema kwamba wamepoka taarifa hiyo na wanamsubiri Mwenyekiti wao wa Bodi, Mohamed 'Mo' Dewji aitishe kikao, lakini wanaamini kila kitu kitakwenda sawa.
Jan 31, mwaka jana Simba SC ilimuuza Kichuya klabu ya Pharco ya Daraja la Kwanza ambayo ilimpeleka kwa mkopo ENPPI ya Ligi Kuu ya Misri.
Hata hivyo, baada ya msimu Kichuya alitakiwa kurejea Pharco na ndipo alipotofautiana na klabu yake hiyo, kabla ya kuripotiwa kurejea Simba SC Januari mwaka huu, ambayo nayo baada ya nusu msimu ikaachana naye akaibukia Namungo FC.

0 comments:
Post a Comment