MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube, leo Alhamisi amefanyiwa upasuaji uliofanikiwa wa kuunga mfupa wa mkono wake wa kushoto uliovunjika Novemba 25 kwenye mchezo dhidi ya Yanga.
Upasuaji huo amefanyiwa saa nane mchana, ambapo amewekewa chuma ili kusaidia kuunga kwa sehemu iliyovunjika kwenye mkono wake, kitaalamu upasuaji huo unaitwa ORIF = OPEN REDUCTION INTERNAL FIXATION.
Dube anatarajiwa kuwa nje ya uwanja, kwa majuma manne akiuguza jeraha lake hilo.

0 comments:
Post a Comment