// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DKT ABBASI ASEMA SERIKALI INATAKA KUWASAIDIA WASANII KUUZA KAZI ZAO MTANDAONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DKT ABBASI ASEMA SERIKALI INATAKA KUWASAIDIA WASANII KUUZA KAZI ZAO MTANDAONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 17, 2020

    DKT ABBASI ASEMA SERIKALI INATAKA KUWASAIDIA WASANII KUUZA KAZI ZAO MTANDAONI

    Na Shamimu Nyaki – WHUSM, DAR ES SALAAM
    KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  amesema kuwa Serikali katika kukuza na  kuhakikisha maslahi ya wasanii yanaboreshwa, imeanza kupokea mawazo kuhusu namna bora ya  kutumia mifumo ya kiteknolojia  katika kuuza kazi za Sanaa
    Dkt. Abbasi ameyasema hayo Desemba 17, 2020 Jijini Dar es Salaam   alipokuatana na kufanya kikao na wadau wa mifumo ya kuuza kazi za Sanaa ambapo amesema kuwa Serikali inataka kuweka mazingira bora ya kufanya kazi ya Sanaa ambayo itawanufaisha na kuwasaidia kupata soko la uhakika huku akisistiza kuwa mifumo ambayo wadau watapendekeza   lazima iwe bora katika kuonyesha maudhui na yenye viwango bora.
    “Wasanii mnapaswa kutumia teknolojia ambayo kwa sasa ndio inabeba soko la kuuza n kazi zenu, na lazima mtambue kuwa “teknolojia huwezi kushindana nayo ila unaweza kufaidika nayo”   hivyo ni jukumu lenu kutumia fursa hiyo”,alisema Dkt.Abbasi.
    Aidha, Dkt. Abbasi amewataka wabunifu na wasanii wote kusajili kazi zao katika Taasisi ya Hakimili Tanzania (COSOTA) ili zilindwe na Sheria ambazo zinasimamiwa na Serikali lengo likiwa ni kuwanufaisha wasanii hao.


    Vilevile, Dkt. Abbasi   amewaagiza wasanii hao na wadau wote wa Sanaa kuwasilisha serikalini tozo zote ambazo zimekuwa ni kero katika kutekeleza kazi zao ifikapo Desemba 31, 2020 ili Serikali izifanyie kazi.
    Naye Bw. Lumuliko Mengele kutoka Kampuni ya Blackball ameishukuru Serikali kuona umuhimu wa kutumia mifumo   katika kuuza kazi za Sanaa ambapo ameshauri kuwa mifumo hiyo iwe na uwanja mpana katika kufanya kazi hiyo.
    Kwa upande wake Bw.Emmanuel Godfrey  ameshauri kuwa mifumo itakayoridhiwa lazima iwekewe vigezo ambayo watumiaji wengi watakuwa na uwezo wa kuvifikia huku akisistiza kuwa Serikali iiratibu mifumo hiyo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DKT ABBASI ASEMA SERIKALI INATAKA KUWASAIDIA WASANII KUUZA KAZI ZAO MTANDAONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top