Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BONDIA maarufu, Abdallah Pazy “Dulla Mbabe” ameondolewa kuzipiga na
bondia kutoka DR Congo Alex Kabangu na nafasi yake imechukuliwa na Hussein
Itaba.
Pambano hilo limepangwa kufanyika Novemba 13 kwenye ukumbi wa Next Door
Arena, Oysterbay na ambapo siku hiyo pia bondia nyota nchini Hassan Mwakinyo
atapigana na bondia Jose Carlos Paz kutoka Argentina akiwania mikanda miwili.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Jackson Sport, Kelvin Twissa alisema jana
kuwa mabadiliko hayo ni kawaida kutokea katika masuala ya ngumi za kulipwa
bondia huyo (Itaba) ameanza mazoezi kwa ajili ya kupambana na Kabangu.
Hivi karibuni, Mbabe alipigwa kwa pointi dhidi ya bondia Bek Nurmaganbet mjini Atyrau, Kazakhstan.
Bondia huyo alikwenda kupigana chini ya promota Jay Msangi.
“Tumeona tufanye mabadiliko katika moja ya pambano letu kwa lengo la
kupanua wigo na kujenga heshima katika ngumi za kulipwa nchini, hivyo
mabadiliko hayo yamefanywa ili kupanua wigo wa mabondia na kuinua vipaji zaidi
hapa nchini, naamini Itaba atafanya vyema katika pambano hilo,” alisema Twissa.
Alisema kuwa maandalizi ya mapambano ya ‘Dar Fight Night’ yanaendelea
vizuri huku bondia bingwa wa mabara wa uzito wa superwelter Hassan Mwakinyo
akijifua vikali.
Mbali ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara wa uzito huo huo wa Chama cha IBA.
Mabondia kutoka nchi tano watazichapa kumsindikiza Mwakinyo na Paz,
akiwamo aliyekuwa bingwa wa dunia wa WBC, Fatuma Zarika kutoka Kenya. Zarika
atazichapa na Patience Mastara wa
Zimbabwe, na Zulfa Yusuph Macho atacheza na Alice Mbewe wa Zimbabwe.
Alisema kuwa wameamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi kutokana na kutambua
vipaji vya mabondia mbalimbali hasa Mwakinyo ambaye anafanya vizuri katika
mapambano yake.
"Siku hiyo kutakuwa na pambano
makubwa ambapo mabondia kutoka nchi sita, Argentina, DR Congo, Kenya,
Zimbabwe na wenyeji Tanzania watapigana, ni siku ambayo mashabiki wa ngumi za
kulipwa wataona kitu tofauti kabisa katika mchezo huo, " alisema Twisa.
Alisema kuwa kampuni yao chini ya udhamini wa Azam TV, colosseum hotel
Dar es salaam na Asas ina uzoefu mkubwa
katika kuandaa matamasha, masoko na shughuli mbalimbali na kuahidi kufanya
jambo la kihistoria hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment