// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAAHIDI KUYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YA YANGA SC JUU YA MKATABA WA SIMBA NA MORRISON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAAHIDI KUYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YA YANGA SC JUU YA MKATABA WA SIMBA NA MORRISON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 02, 2020

    TFF YAAHIDI KUYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YA YANGA SC JUU YA MKATABA WA SIMBA NA MORRISON

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

    SHIRIKISHO la Soka Tanzana (TFF) limesema limepokea malalamko ya klabu ya Yanga juu ya mapungufu ya mkataba wa winga Mghana, Bernard Morrison na Simba SC na utayafanyia kazi kwa mujibu wa taratibu.

    Yanga SC jana iliwasilisha malalamiko TFF, ikitaka mahasimu wao, Simba wapokwe pointi zote kwenye mechi ambazo Morrison amecheza, kwa sababu mkataba baina yao una mapungufu na haujapitishwa katika mfumo wa usajili (TMS) wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FFA).

    Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwalalebela alidai mkataba huo una sahihi moja tu na kwa ujumla mkataba ambao upo kwenye Mfumo wa Usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kati ya Simba na Morrison umesainiwa na upande mmoja tu, wa mchezaji.


    Yanga imelalamika mkataba wa Bernard Morrison na Simba SC una hitilafu na haujapitishwa FIFA 





    Pamoja na upande wa Simba kutosaini wala kugonga muhuri, pia hakuna tarehe ya kusaini mkataba huo kati ya pande zote mbili husika na hakuna saini za Kamishina wa Viapo na wala mashahidi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAAHIDI KUYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YA YANGA SC JUU YA MKATABA WA SIMBA NA MORRISON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top