
Mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Ally Samatta (kulia) wa Fenerbahce akimtoka beki wa kimataifa wa Bosnia na Herzegovina wa klabu ya Goztepe SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki leo Uwanja wa Goztepe Gursel Aksel Jijini İzmir. Fenerbahce imeshinda 3-2, mabao yake yakifungwa na José Ernesto Sosa kwa penalti dakika ya 26, Serdar Aziz dakika ya 43 na Dimitris Pelkas dakika ya 51, wakati ya Goztepe SC yote yamefungwa na Guilherme kwa penalti pia dakika ya 34 na lingine dakika ya 63 akimalizia pasi ya Halil Akbunar.

0 comments:
Post a Comment