Manchester United imepangwa Kundi la Kifo katika Lig0 ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU ya Manchester United ya England imepangwa katika kundi gumu kwenye msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kimewekwa Kundi H pamoja na wana fainali, Paris Saint-Germain ya Ufaransa, RB Leipzig ya Ujerumani na Istanbul Basaksehir ya Uturuki.
Kundi A linazikutanisha bingwa mtetezi, Bayern Munich ya Ujerumani, Atletico Madrid ya Hispania, RB Salzburg ya Ujerumani na Lokomotiv Moscow ya Urusi.
Kundi B kuna Real Madrid ya Hispania, Shakhtar Donetsk ya Uturuki, Inter Milan ya Italia na Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.
Kundi C; Porto ya Ureno, Manchester City ya England, Olympiacos ya Ugiriki na Marseille ya Ufaransa.
Kundi D kuna Liverpool ya England, Ajax ya Uholanzi, Atalanta ya Italia na Midtjylland ya Denmark.
Kundi E kuna Sevilla ya Hispania, Chelsea ya England, Krasnodar ya Urusi na Rennes ya Ufaransa.
Kundi F zipo Zenit ya Urusi, Borussia Dortmund ya Ujerumani, Lazio ya Italia na Club Brugges ya Ubelgiji.
Kundi G zipo Juventus ya Italia Barcelona ya Hispania, Dynamo Kyiv ya Ukraine na Ferencvaros ya Hungary.
Kundi H ndio; Paris Saint Germain, Manchester United, RB Leizpig na Istanbul Basaksehir.
Fainali ya msimu huu itafanyika Mei 29, mwakani Uwanja wa Ataturk Jijini Istanbul, ambako Liverpool ilifanya maajabu ya kutosahaulika baada ya kutoka nyuma kwa 3-0 na kuifunga AC Milan kwa penalti mwaka 2005.
0 comments:
Post a Comment