Na Asha Said, DAR ES SALAAM
VIGOGO, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, Mlandege SC katika mchezo wa kirafiki usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Ulikuwa mchezo maalum wa kujiandaa na mechi yao ijayo ya Ligi Kuu ya Tanzanka Bara Jumamosi Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Na kocha Mserbia wa Yanga SC, Zlatko Krmpotic alitumia wachezaji 22, akianza na 11 kipindi cha kwanza na wengine kipindi cha pili na kila kikosi kilipata ushindi wa 1-0.
Kikosi kilichoanza kikiongozwa na Nahodha, kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima bao lake lake lilifungwa na mshambuliaji mpya, Waziri Junior kwa mkwaju wa penalti dakika ya 40.
Na kikosi kilichoingia kikiongozwa na Nahodha, Deus Kaseke bao lake lilifungwa na kiungo mpya, Tonombe Mukoko kutoka AS Vita ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa shuti kali dakka ya 59 baada ya kutengewa pasi na mshambuliaji mpya, Mburkinabe, Yacouba Sogne aliyesajlwa kutoka Asante Kotoko ya Ghana.
Mlandege SC ilimaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Ibrahim Ali Juma kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 75.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata/Ramadhan Kabwili dk46, Kibwana Shomari/Deus Kaseke dk46, Adeyum Ahmed/Yassin Mustapha dk46, Said Juma ‘Makapu’/Lamine Moro dk46, Abdallah Shaibu ‘Ninja’/Bakari Mwamnyeto dk46, Abdulaziz Makame/Tonombe Mukoko dk46, Ditram Nchimbi/Zawadi Mauya dk46, Feisal Salum/Carlos Carlinhos dk46, Waziri Junior/Michael Sarpong dk46, Haruna Niyonzima/Yacouba Sogne dk46 na Farid Mussa/Tuisila Kisinda dk46.
0 comments:
Post a Comment