• HABARI MPYA

        Wednesday, September 16, 2020

        PRINCE DUBE AFUNGA TENA LAKINI AZAM FC YACHAPWA MABAO 2-1 NA TRANSIT CAMP CHAMAZI

        MSHAMBULIAJI mpya, Mzimbabwe, Prince Dube (kushoto) na leo amefunga kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp ya Daraja la kwanza, lakini Azam FC imechapwa 2-1 Uwanja wa pili wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

        Mabao ya Transit Camp inayomilikwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambayo inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara yamefungwa na Abdallah Kheri aliyejifunga na Damas Makwaya.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: PRINCE DUBE AFUNGA TENA LAKINI AZAM FC YACHAPWA MABAO 2-1 NA TRANSIT CAMP CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry