Na Agnatius Obel, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amejiunga na Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Aston Villa ya England.
Kwa mujibu wa www.expressandstar.com, Samatta mwenye umri wa miaka 27 anakwenda kucheza Uturuki kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu atakapouzwa moja kwa moja kwa ada ya Pauni Milioni 5.5 kumalizia mkataba wake wa Villa.
Samatta alijiunga na Aston Villa Januari mwaka huu kwa dau la Pauni Milioni 10 kutoka klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akisaini mkataba wa miaka minne na nusu.
Amecheza mech 14 tu hadi sasa na kufunga mabao mawili – Aston Villa ikichapwa 2-1 na wenyeji, AFC Bournemouth mechi ya Ligi Kuu alifunga kwa kichwa dakika ya 70 Uwanja wa Vitality.
Siku hiyo AFC Bournemouth iliyomaliza pungufu baada ya Jefferson Lerma kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 51, ilitangulia kwa mabao ya kiungo wa kimataifa wa Denmark, Philip Billing dakika ya 37 na beki Mholanzi, Nathan Ake dakika ya 44.
Samatta akafunga tena bao la kufutia machozi Aston Villa ikichapwa 2-1 na Manchester City katika fainali ya Kombe la Ligi England Uwanja wa Wembley Jijini London.
Manchester City inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pep Guardiola ilitangulia kwa mabao ya mshambuliaji wake tegemeo, Muargentina Sergio Aguero dakika ya 20 akimalizia pasi ya Philip Foden na Rodri Hernandez akimalizia pasi ya İlkay Gundogan dakika ya 30.
Akiwa ana umri wa miaka 27 sasa, Samatta aliibukia klabu ya African Lyon wakati ikiitwa Mbagala Market ya kwao, Mbagala kabla ya kujiunga na Simba SC, zote za Dar es Salaam na baadaye TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo ndiyo haswa ilimkuza kisoka kabla ya kuhamia Ulaya mwaka 2016.
Akiwa Genk, Samatta ambaye sasa ndiye Nahodha wa Taifa Stars, alifunga mabao 76 katika mechi 191 hadi Aston Villa kuvutiwa naye na kumnunua.
Kumekuwa na mitazamo tofauti juu ya Samatta kuondolewa Aston Vlla baada ya nusu msimu tu, lakini kwangu mimi hii ni Cheap Argument. Poppa kafeli.
Its seems tuko alert na matukio. Andrey Shevchenko kushindwa kucheza Chelsea haikuwa big deal. Juan Sebastian Veron kushindwa kucheza Manchester United haikuwa big deal pia.
Mifano ni mingi na pia Samatta angefanikiwa ingemaanisha nini kwenye soka letu directly.....!?
Or leo mchezaji akienda kucheza Ulaya akitokea hapa Tanzania itamaanisha nini kwenye soka letu directly......!?
Msanii anayefanya vizuri kwa sasa ni Diamond Platnumz, natumai mwanzo wa Safari yake, hakuna ambaye angeona Diamond anafika hii stage
Nonda Shaaban Papii, tunaweza kusema ni Mchezaji ambaye amewahi kupita Ligi ya Tanzania na akafanikiwa Ulaya, lakini hakuna hata mmoja angeona Credentials hizo ahead of Mohammed Hussein, Kizota na Lunyamila....et al, na kutoka kwake hapa home hakukumanisha chochote
Edward Maka na Simon Msuva wanacheza Ligi ya Morocco moja ya Ligi Bora Africa, lakini mtoto wa Zidane ambaye ana msingi wa kukulia Ulaya katika mafunzo ya hali ya juu, ameshindwa kucheza Ulaya na anarudi Morocco kucheza Ligi moja na akina Maka na Msuva hii haiwezi kuwa big deal
Back to your concern, nadhani wote tulimuona Michael Olunga alipokuja na Gor Mahia, kwa kutazama mpira huwezi kumuweka Olunga katika viwango vya kutisha kiasi kwamba tungemtabiria mengi, Olunga kacheza Ligi ya Spain na sasa yuko China anatisha na kukusanya kitabu...
Kuwasifia wageni wanaocheza hapa, kusema ni sifa za kijinga just kwamba unaweka notion kwamba wangekuwa wazuri basi wangecheza Ulaya, naweza kusema ni hisia kali katika kitu usichopenda kuona sawa sawa na matamanio yako
Kama wanafanya vizuri kuliko wengine ache wapate sifa, kama wanapewa sifa zisizostahili ili hali kuna watu wanawazidi hapa hapa nyumbani, hiyo ni hoja yenye Ujazo mkubwa....
Mpira hautabiriki, mpira hauna kauli za kusema haiwezekani, au kitu chochote kinachohusu Talent.....
Kucheza Mpira Ulaya ni mchanganyiko wa mambo mengi mno, kuliko vile tunavyoviona katika upeo wa mwanzo wa macho yetu....
Nimesema Nonda kacheza Ulaya kwa kufanikiwa....
Ila chukua watu waliwaona Nonda na Lunyamila, waambie kwamba Nonda alifanikiwa kucheza Ulaya ila Lunya alishindwa kucheza hata Lower Division wasikie watakuambia nini, ndio hapo utajua nini namaanisha
Olunga haingii hata Robo ya Lunya, lakini kacheza La Liga na sasa anavuna Utajiri huko China
Sisi watanzania tunapenda sana matukio....
Edward Maka na Ally Msengi, wanacheza Morocco na SA, hawajawahi hata kuwa na full season katika VPL na wameweza kucheza huko
Ibrahim Ajib, Mkude na wengineo walishindwa kupata nafasi kucheza Ligi ya South....
Abdi Banda alitakiwa na kacheza, pamoja na Ngassa akiwa mwishoni...
Tunawaza sana Shortcut, tunawaza sana kwamba ikiwa hivi basi ni vile....
No kuna kazi ya kufanya hadi kufanikiwa, sisi tuna Samatta tu, nchi nyingine zina kina Samatta 100 na wanaofanikiwa labda ni 50, kwa hiyo huwezi kuona tofauti...
ilifika kipindi watu wanaaminia Samatta ni mchezaji mwenye kipaji mno kuwahi kutokea Tanzania, ni kwa sababu tuliamua kufunga mawazo kwake...
Na anayesema Samatta is failure, basi huu Mpira uendelee kuitwa mchezo wa wazi na washabiki wawe ndio Uzio.
(Mwandishi wa makala hii ni mdau wa soka anayepatikana kwa nambari +255 756 798 313)
0 comments:
Post a Comment