Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO wa Simba SC, Clatous Chotta Choma atawania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya mabeki Nicolas Wadada wa Azam FC na Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union.
Sherehe za tuzo za Ligi Kuu zitafanyika Jumamosi wiki hiii katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kuonyeshwa LIVE na Azam TV kupitia chaneli ya Azam Sports 2.
Katika orodha iliyotolewa na Bodi ya Ligi jana, Chama pia atawania tuzo ya Kiungo Bora dhidi ya Lucas Kikoti wa Namungo FC na Mapinduzi Balama wa Yanga SC.
Mlinda mlango namba moja Tanzania, Aishi Salum Manula atachuana na Mburkina Faso, Nourdine Balora wa Namungo FC na Daniel Mgore wa Biashara United ya Mara katika kuwania tuzo ya Kipa Bora.
Mlinzi Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union atachuana na David Luhende wa Kagera Sugar na Nico Wadada wa Azam FC katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Beki Bora,
Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi imewakutanisha Kelvin Kijiri wa KMC, Dickson Job wa Mtibwa Sugar na Novatus Dissmas wa Biashara United.
Tuzo ya Bao Bora inashindaniwa na Sadallah Lipangile wa KMC kwa bao lake alilofunga dhidi ya Mtibwa Sugar, Luis Miquissone wa Simba SC bao alilofunga dhidi ya Alliance na Patson Shikala wa Mbeya City bao alilofunga dhidi ya JKT Tanzania.
Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck wa Simba SC anawania tuzo ya Kocha Bora dhidi ya Mrundi Hitimana Thiery wa Namungo FC na Mromania Aristica Cioaba wa Azam FC.
Tuzo ya Mwamuzi Bora inawaniwa na Ahmed Arajiga wa Manyara, Ramadhan Kayoko wa Dar es Salaam na Abdallah Mwinyimkuu wa Singida, wakati Mwamuzi Msaidizi wapo Frank Komba wa Dar es Salaam, Abdulaziz Ally wa Arusha na Hamdani Said wa Mtwara. Timu yenye Nidhamu; Coastal Union, Kagera Sugar na Mwadui FC.
Ikumbukwe Mfungaji Bora ni Meddie Kagere wa Simba aliyemaliza na mabao 22, mbele ya Yussuf Mhilu wa Kagera Sugar na Peter Mapunda wa Mbeya City mabao 13 kila mmoja, Waziri Junior wa Mbao FC mabao 12 sawa na Mzambia Obrey Chirwa wa Azam FC na Reliant Lusajo wa Namungo FC.

0 comments:
Post a Comment