Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic akishangilia na Franck Kessie baada ya AC Milan kutoka nyuma na kuichapa Juventus 4-2 katika mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan. Mabao ya AC Milan yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 62, Franck Kessie dakika ya 66, Rafael Leao dakika ya 67 na Ante Rebic dakika ya 80 baada ya Juventus kutangulia kwa mabao ya Adrien Rabiot dakika ya 47 na Cristiano Ronaldo dakika ya 53. Kwa ushindi huo, AC Milan inafikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 31 na kuoanda kwa nafasi mbili hadi ya tano, sasa ikizidiwa pointi 14 na Atalanta inayoshika nafasi ya nne, wakati Juventus inabaki kileleni na pointi zake 75, sasa ikiizidi saba Lazio baada ya wote kucheza mechi 31 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Ghana forward Inaki Williams leads Athletic Bilbao as Top scorer and
assister
-
Inaki Williams continues to make his mark at Athletic Bilbao, remaining one
of the team's most influential players.The Ghanaian international is tied
as th...
22 minutes ago
0 comments:
Post a Comment