// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA CHUPUCHUPU KUPIGWA NA MTIBWA SUGAR GAIRO, MBAO YAITANDIKA NAMUNGO 3-0 KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA CHUPUCHUPU KUPIGWA NA MTIBWA SUGAR GAIRO, MBAO YAITANDIKA NAMUNGO 3-0 KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, July 22, 2020

    YANGA CHUPUCHUPU KUPIGWA NA MTIBWA SUGAR GAIRO, MBAO YAITANDIKA NAMUNGO 3-0 KIRUMBA

    Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
    VIGOGO, Yanga SC wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
    Sare hiyo inayoiongezea pointi moja kila timu, inaifanya Yanga SC ifikishe pointi 69 baada ya kucheza mechi 37 na kuendelea kukamata nafasi ya pili nyuma ya mabingwa tayari, Simba SC wenye pointi 84 za mechi 36. 
    Mtibwa Sugar inabaki nafasi ya 14 pamoja na kufikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 37, ikiipisha Mwadui FC ipande kwa nafasi tatu hadi ya 13 baada ya kuichapa 1-0 Biashara United leo.

    Katika mchezo wa leo Gairo, Mtibwa Sugar walitangulia kwa bao la kiungo wake Haruna Chanongo dakika ya 27, kabla ya beki Adeyoum Ahmed kuisawazishia Yanga SC dakika ya 82.   
    Mechi nyingine za leo, bao pekee la Mussa Chambenga dakika ya 90 na ushei limetosha kuipa Mwadui FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga.
    Nayo Mbao FC ikaichapa 3-0 Namungo FC mabao yake yakifungwa na Jordan John dakika za nne na 14 na Abdulkarim Segeja dakika ya 28 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Bao pekee la Ramadhani Ibata dakika ya 85 likaipa ushindi wa ugenini wa 1-0 Tanzania Prisons dhidi ya wenyeji, KMC Uwanja wa Azam Complex, Chamaz nje kdogo ya Jiji la Dar es Salaam.
    Nao Kagera Sugar wakapata ushindi wa 2-1 ugenini pia dhidi ya Singida United Uwanja wa Liti, zamani Namfua. Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Kelvin Sabato dakika ya nne Awesu Awesu dakka ya 52.
    Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed Nduda, Kibwana Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Dickson Job, Dickson Daudi, Abdulhalim Humud, Ally Makarani, Jaffar Kibaya, Salum Kihimbwa na Haroun Chanongo. 
    Yanga SC; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Adeyoum Ahmed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Ally Mtoni ‘Sonso’, Abdulaziz Makame/ Tariq Seif dk80, Feisal Salum, Deus Kaseke, David Molinga/ Mrisho Ngassa dk57 na Yikpe Gislain.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA CHUPUCHUPU KUPIGWA NA MTIBWA SUGAR GAIRO, MBAO YAITANDIKA NAMUNGO 3-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top