Na Mwandishi Wetu, MTWARA
MABINGWA, Simba SC wamelazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Ndanda SC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania jioni ya leo.
Sare hiyo inaifanya Simba SC ifikishe pointi 80 baada ya kucheza mechi 33, sasa ikiwazidi pointi 19 vigogo, Yanga SC wanaofuatia katika nafasi ya pili.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Yanga SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Nayo Alliance FC imelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, wenyeji wakitangulia kwa bao la kujifunga la Henry Joseph dakika ya kwanza kabla ya Salum Kihimbwa kuwasawazishia wagen dakika ya 55.
Kikosi cha Ndanda SC kilikuwa; Ally Mustapha ‘Barthez’, Swaleh Abdallah, Hemed Khoja, Abdulrazack Mohamed, Paul Maona, Donald Taro, Abdul Hamisi, Hussein Javu, Omar Mponda/Omar Ramadhani dk75, Vitalis Mayanga/Kassim Mdoe dk81 na Kiggi Makasi.
Simba SC; Aishi Manula, Haruna Shamte, Gardiel Michael, Kennedy Juma, Pascal Wawa/Erasto Nyoni dk67, Jonas Mkude, Deo Kanda, Gerson Fraga ‘Viera’/Muzamil Yassin dk69, John Bocco, Clatous Chama na Luis Miquissone/Hassan Dilunga dk69.

0 comments:
Post a Comment