Na Mwandishi Wetu, LIVERPOOL
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza kwa dakika 63, Aston Villa ikilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Everton Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool.
Samatta, mchezaji wa zamani wa African Lyon na Simba za Tanzania, alitoka dakika ya 63 kumpisha KeinanDavis, wakati huo timu hizo bado hazijafungana.
Na akiwa benchi, Samatta akashuhudia Aston Villa ikitangulia kwa bao la Ezri Konsa dakka ya 72 akimalizia pasi ya Conor Hourihane kabla ya Theo Walcott kuisawazishia Everton dakika ya 87 akimalizia pasi ya Andre Gomes.
Sasa Aston Villa inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 36, ingawa inabaki nafasi ya 19, ikizidiwa wastani wa mabao tu na AFC Bournemouth inayoshika nafasi ya 18.
Kikosi cha Everton kilikuwa: Pickford, Coleman, Keane, Holgate/Branthwaite dk15, Digne, Iwobi/Walcott dk61, Gomes, Davies, Bernard/Gordon dk61, Richarlison/Kean dk73, Calvert-Lewin.
Aston Villa: Reina, El Mohamady, Konsa, Mings, Targett, McGinn, Luiz, Hourihane, Trezeguet/El Ghazi dk63, Grealish, Samatta/Davis dk63.

0 comments:
Post a Comment