Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
KADHIA ya usafiri ni jambo ambalo haliepukiki hasa kwa wakazi walio wengi wa Dar es salaaam.
Safari yangu ya dakika takribani 25,kutoka maeneo ya Ilala Shariff Shamba kuelekea maeneo ya Buguruni chama ilikamilika.
Nikiwa hapo kama mmoja kati ya Abiria waliokuwa katika kituo hicho kusubiria magari ya kuelekea nyumbani kwetu mbagala.
Ilikuwa ni siku ambayo ni kama magari yalizuiliwa kwani hadi majira ya saa 4 usiku hakuna mtu yeyote kati ya abiria wengi tuliokuwa kituoni hapo aliyekwisha kupata gari.
Pembeni ya stend hiyo kulikuwa na kijiwe cha kahawa kilichokuwa kitupu,nilimshuhudia mzee mmoja akijongea katika eneo hilo na kuchukua nafasi yake ya kukaa,kwakuwa miguu ilishaanza kuchoka nami nikajongea hapo na baada ya muda kijiwe kikawa kimefikiwa na watu wengi waliokuwa wanataka huduma ya kinywaji adhimu cha kahawa kutokana na kibaridi kilichokuwa kimeanza stendi hapo.
Kijana mmoja ambaye makadirio yake ya miaka ilikuwa kati ya miaka 18 hadi 19 alifungua mjadala ambao ulikuwa wamotom kweli kweli.
"Tofauti kati ya mlipili na mabeki wengine wa kati hapa nchini ni bahati tu,lakini mlipili ni bonge la beki wa kati"
Aikuchukua sekunde hata kumi kuelewa kauli ya kijana huyu,kauli ambayo niliiona kuwa imejaa ukweli ulioshiba na kunenepa ndani ya herufi zinazounda kauli yake hii.
Waswahili wanasema Jua haliwaki Usiku na hii ni kutokana kwamba sio kwamba halina uwezo wa kuwaka bali kwa kawaida Usiku ni wakati wa mwezi kuwaka kwakuwa jua liliwaka mchana.
Mlipili huyu ambaye alisimama vilivyo kipindi Irambona masood djuma anaachiwa kikosi kutoka kwa Joseph omog kabla ya kuletwa mfaransa lechantre.
Midomo ya mashabiki inaonekana kuwa haimsemi tena na kusahau kabisa kama wana mchezaji Ambaye aliimfanya Aishi Manula awe likizo kila anapokuwa anakanyaga nyasi za uwanja wa mpira wa miguu alafu mbele yake akamshuhudia Milipili na tatoo yake.
Kwenye maisha kuna mda licha ya kuwa na jitihada lakini pia unahitaji bahati ili uweze kufanikiwa,Mlipili kwenye hili ni dhahiri namuona kuwa amekosa bahati licha ya kuwa na kipaji.
Anabaki anaishi huku akiwa hajui hatma yake ni nini ndani ya kikosi hicho.
Pengine nguvu humuisha zaidi pale anapo muangalia Tairone santos ambaye amesafiri safari ndefuu kutoka bara moja hadi nyengine kuja kucheza eneo ambalo yeye anacheza.
Pindi nimuangaliapo mchezaji huyu huwa siishiwi maswali kichwani mwangu.Huku moja ya swali ambalo hunijia kichwani ni kiwango anacho kionesha beki huyu wa kati wa hapa nchini kwetu na kiwango cha huyu ambaye amesafiri kutoka bara moja hadi jengine.
Nina hakika Mlipili ni moja ya mabeki bora kabisa kama atapewa nafasi ya kucheza.
Ila shida kubwa ni kwamba nguvu ya Umma nayo haioneshi kumsapoti.Sio ambaye anasemwa kama alivyosemwa Juuko mursheed,naliona jembe hili likiwa linazidi kuliwa na kutu na tusipokuwa makini tutakufa njaa kwani baada ya muda fulani jembe hili litamalizwa na kutu na wakati tunakuja kukumbuka kulilimia tutakuta halina uwezo tena wa kulimiwa kutokana na kuto tumiwa mda mrefu.
Jembe hili endapo litamalizwa na kutu hii haitakuwa ni Njaa ya Klabu ya Simba tu.bali itakuwa ni njaa ya Taifa zima kwani naamini kesho tungemtumia Mlipili badala ya Yondani ambaye anaonekana kuchoshwa na safari za Ndege kila inapokuja Ratiba ya FIFA na CAF hata kuna kipindi akaamua kuomba kuondoka,lakini kwakuwa hatukuwa na utaratibu wa kuyatumia Majembe yetu kama huyu Mlipili tukaamua kumuomba asiondoke ili kusaidia Jahazi lisizame.
Macho madogo yaliyopambwa na taswira ya machozi pamoja na kiwango alichowahi kukionesha chini ya Masood Djuma ndio vitu pekee vitakavyo mfanya Mlipili pengine tumuone akirudi tena kwenye vioo vya runinga zetu tena.
Kuna mda huwa nawaza pengine mlipili anakosa watu sahihi wanao msimamia au bado anaona Taabu kuziacha posho za MO,yoote huenda yakawa majibu lakini bado kwangu namuona Mlipili akienda Kung'ara kwenye kikosi chochote kwenye ukanda wetu huu wa Afrika ya Mashariki.
Matamanio yake ya mpira anapokuwa uwanjani ndio miongoni mwa vitu vinanvyo nifanya niamini kwamba Mlipili bado ubongo wake una njaa ya kuona anapeana mikono huku kifuani akiwa na bendera ya Taifa lake pendwa la Tanzania.
Bado ana uwezo lakini shida hatutambui uwezo wake,mwisho nabaki kusema tu kuwa MLIPILI ni jembe linaloota kutu.mpaka namaliza kufikiria tayari kahawa na ilikwishaisha na gari ilishawasili kituoni hivyo nikanonge kupanda gari hilo kisha nikaachana na ya Mlipili.
@Mustafa.mtupa

0 comments:
Post a Comment