Na Mwandishi Wetu, İZMIR
TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Tanzania leo imeshinda mechi ya kwanza kwenye michuano maalum ya kimataifa ya Marcedes Benz Aegean Cup inayoendelea nchini Uturuki baada ya kuichapa Kosovo 4-2.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Altınordu Jijini İzmir, mabao ya Tanzania yalifungwa Ladak Juma dakika ya 13, Kassim Ibrahim dakika ya 16 na Omar Abbas mawili dakika ya 39 na 67.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza Tanzania inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Maji Maji ya Songea, Maalim Saleh ‘Romaro’ ilifungwa 1-0 na Ireland.
Na kikosi hicho kilichoongozana na kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya wakubwa, Mrundi Etienne Ndayiragije kitacheza mechi yake ya mwisho keshokutwa dhidi ya wenyeji, Uturuki.
Ifahamike Tanzania ipo Kundi A pamoja na wenyeji Uturuki, walioshinda 1-0 mara mbili kwenye mechi zake za awali dhidi ya timu nyingine za kundi hilo, Kosovo na Ireland.

0 comments:
Post a Comment