// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KMC YAWAADHIBU MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI, YAWATANDIKA MTIBWA SUGAR 2-0 DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KMC YAWAADHIBU MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI, YAWATANDIKA MTIBWA SUGAR 2-0 DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, January 17, 2020

    KMC YAWAADHIBU MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI, YAWATANDIKA MTIBWA SUGAR 2-0 DAR

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
    Ushindi huo unaifanya KMC ifikishe pointi 17 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya 17 wakati Mtibwa Sugar inafikisha pointi zake 22 baada ya kucheza mechi 16 na inabaki nafas ya 10.
    Katika mchezo wa leo, mabao ya KMC inayocheza Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo tangu ipande, yote yamefungwa Sadallah Lipangile dakika ya 18 akimalizia pasi ya Serge Tapei na la pili dakika ya 41 akimalizia pasi ya Ally Ramadhani.
    Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha Zubery Katwila inapoteza mchezo huo wa Ligi Kuu ikitoka kufanya vyema kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kubeba taji hilo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba kwenye fainali Jumatatu wiki hii Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Kikosi cha KMC Kilikuwa; Jonathan Nahimana, Ismail Gambo, Ally Ramadhani, Abdallah Mfuko, Jean Baptiste Mugiraneza, Kenny Ally, Hassan Kabunda/Kelvin Kijiri dk65, Emmanuel Mvuyekure, Sadallah Lipangle/Salim Aiyee dk85, Suleman Ndikumana na Serge Alian.
    Mtibwa Sugar; Shaaban Kado, Kibwana Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Dickson Job, Cassian Ponera, Abdulhalim Humud, Awadh Salim/Haruna Chanongo dk46, Ally Makarani, Jaffary Kibaya, Onesmo Mayaya/Riphat Khamis dk52 na Salum Kihimbwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KMC YAWAADHIBU MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI, YAWATANDIKA MTIBWA SUGAR 2-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top