// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIUNGO WA ZAMANI WA YANGA NA SIMBA, ALLY YUSSUF ‘TIGANA’ AFARIKI DUNIA LEO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIUNGO WA ZAMANI WA YANGA NA SIMBA, ALLY YUSSUF ‘TIGANA’ AFARIKI DUNIA LEO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 05, 2019

    KIUNGO WA ZAMANI WA YANGA NA SIMBA, ALLY YUSSUF ‘TIGANA’ AFARIKI DUNIA LEO DAR

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ally Yussuf Suleiman ‘Tigana’ amefariki dunia leo katika hospitali ya Amana mjini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.
    Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu, Mwanamtwa Kihweli msiba upo nyumbani kwao Msasani na mazishi yatafanyika makaburi ya Msasani kesho Saa 10:00 jioni.
    “Mkewe alikuwa anaumwa ikabidi akarudi kwao Ilala, naye akaja kumuona mkewe juzi ndio ghafla akaanza kuumwa tumbo la kuhara akapelekwa Amana hadi umauti umemkuta leo,”amesema Kihwelo ambaye amecheza pamoja na Tigana, Yanga, Simba kote mara mbili na Cadets ya Mauritius. 

    Ally Yussuf ‘Tigana’ (kulia) amefariki dunia leo katika hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam 

    Tigana alizaliwa mwaka 1970 Ilala mjini Dar es Salaam na amekulia Mtaa wa Saadani huku akisoma shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambako ndiko alianzia soka kama kipa na baadaye mchezaji wa ndani.
    Timu yake ya kwanza ni Shaurimoyo Kids kabla ya kujiunga na Manyema Rangers mwaka 1989 ambako alicheza hadi mwaka 1991 alipochukuliwa na Pan Africans ikiwa Daraja la Pili (sasa Daraja la Kwanza) wakaipandisha Ligi Kuu mwaka 1993.
    Mwaka 1994 akachukuliwa na Yanga SC ambako alicheza kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Simba SC alikocheza hadi mwaka 1997 akaenda Cadets ya Maurtius alikocheza hadi mwaka 2000 aliporejea Simba SC.   
    Alicheza kwa msimu mmoja Simba SC kabla ya kurejea Yanga SC ambako alicheza hadi mwaka 2004 alipokwenda kumalizia soka yake Twiga SC ya Kinondoni. Jina la Tigana alipewa kutokana na kufananishwa na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa miaka ya 1980, Jean Pierre Tigana.
    Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ally Yussuf Suleiman ‘Tigana’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIUNGO WA ZAMANI WA YANGA NA SIMBA, ALLY YUSSUF ‘TIGANA’ AFARIKI DUNIA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top