Na Mwandishi Wetu, IRINGA
TIMU ya Lipuli FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC jioni ya leo Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Shujaa wa Lipuli FC ‘Wana Paluhengo’ leo alikuwa ni mshambuliaji Daruwesh Saliboko aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 46 na 71 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenza, Paul Nonga.
Kwa ushindi huo, Lipuli FC inafikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya nne, sasa ikilingana kwa pointi na wastani wa mabo na Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya tatu.
Mwadui FC baada ya kipigo cha leo katika mchezo wa 10 wakitoka kuwafunga mabingwa watetezi, Simba SC 1-0 Jumatano wanabaki na pointi zao 11 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 11.
Wanawapisha Mtibwa Sugar nafasi ya 10 ambao wamefikisha pointi 12 katika mchezo wa 10 kufuatia sare ya 0-0 na SIngida United leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Singida United pamoja na sare ya ugenini leo, wanaendelea kushika mkia wakifikisha pointi nne katika mchezo wa 10, sawa na Ndanda FC ambayo imecheza mechi saba.
Ligi Kuu ya Tanzania Bara itaendelea kesho kwa mechi nne, mabingwa watetezi, Simba SC wakiwakaribisha Mbeya City FC Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, Ndanda FC wakiwaakribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Polisi Tanzania wakiwa wenyeji wa Alliance FC Uwanja wa Ushirika mjini Moshi na Coastal Union wakiwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

0 comments:
Post a Comment