Ciro Immoble akishangilia baada ya kuifungia Italia mabao mawili dakika ya nane na 33 katika ushindi wa 9-1 dhidi ya Armenia kwenye mchezo wa Kundi J kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Renzo Barbera mjini Palermo. Mabao mengine ya Italia yalifungwa na Nicolo Zaniolo dakika ya tisa na 64, Nicolo Barella dakika ya 29, Alessio Romagnoli dakika ya 72, Jorginho kwa penalti dakika ya 75, Riccardo Orsolini dakika ya 77 na Federico Chiesa dakika ya 81, wakati bao pekee la Armenia limefungwa na Edgar Babayan dakika ya 79. Kwa ushindi huo, Italia ambayo tayari imekwishafuzu Euro ya mwakani, inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 10, sasa wakiizidi pointi 12 Finland inayofuatia katika nafasi ya pili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Giants Rumors: Brian Daboll, Joe Schoen 'Are Not a Duo' amid Hot-Seat Buzz
-
The New York Giants hired both general manager Joe Schoen and head coach
Brian Daboll ahead of the 2022 season, but that reportedly doesn't mean
they will…
10 minutes ago
0 comments:
Post a Comment