Mshambuliaji wa Azam FC, Mrundi Suleiman Ndikumana aliyekuwa majeruhi akifanya mazoezi na wenzake leo kuelekea mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Triangle United Septemba 28 mjini Bulawayo, Zimbabwe
Beki David Mwantika akiuwahi mpira katka mazoezi kuelekea mchezo huo ambao Azam FC wanatakiwa kushinda 2-0 ugenini ili wasonge mbele, baada ya kuchapwa 1-0 nyumbani
Mshambuliaji Muivory Coast, Richard Ella 'Djodi akionyesha ustadi wake mkubwa katika kuumiliki mpira
Mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa akiwa mazoezini leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Mshambuliaji mwingine Mrundi, Emmanuel Mvuyekure akiondoka na mpira dhidi ya Masoud Ally 'Cabaye'
Kiungo mshambuliaji, Iddi Kipagwile akielekeza jambo mazoezini
Lakers Insider: Rob Pelinka 'Trending' to Be This Year's 'Scapegoat' if LA
Loses
-
The Los Angeles Lakers could be in for some changes if they are unable to
get their inconsistent season back on track. The Athletic's Jovan Buha said
durin...
18 minutes ago
0 comments:
Post a Comment