Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
KUNA wakati unawaza hivi wale ambao wanahangaika kutaka kuhama Bongo wanawazaga nini?kwani ukiwaza burudani,utani,mizaha na mbwembwe zimezagaa kila kona,wabongo ni watu fulani maridadi sana,watu wa kikimbiza muda,watu wa mipango ingawa si lazima ikamilike na ikibuma basi fasta kwa lugha ya Mbagala wanahamia mchongo mwingine ili mambo yaende,ukianzia utani wa makabila,kisha unatumbukia kwa wanamuziki na fleva zao ujakaa sawa mara unakutana na Simba na Yanga hapa ndio unatulia na kuvuta kiti,kama utaagiza kahawa,alkasusu,juice,au vile vitu vichungu lakini vinapendwa hiyo wewe tu.
Tuachane na wabongo na madoido yao turudi kwenye mpira wetu,soka letu,ulevi wetu ambapo kuna wakati unapata mauvimu bila kipigo na ukiwa dhaifu mchozi utakutoka tuu.Katika kipindi kitamu cha soka la bongo ni kipindi cha usajili ambapo kuna kuwa na mambo mengi tambo nyingi,misemo mingi na matumaini ya kupitiliza juu ya ubora wa vikosi vya Simba na Yanga ingawa ligi ina timu 20 ila ukifika kwa timu hizi 2 inatakiwa upige breki na uwe na roho pia.Siku za karibu yakaibuka mengine mazito na kuendelea kunakshi mpira wetu na kuzidisha utani wa jadi wa timu hizi mbili kwani kuna kitu au tukio linahitwa WIKI YA MWANANCHI ambayo kimsingi ilitakiwa ianze tarehe 21/7 hadi 27/7 ambayo ndio ingekuwa siku ya kilele ambapo mambo mbalimbali yangeitimishwa katika dimba la Taifa lakini kutokana na muingiliano wa ratiba na michuano ya CHAN ikabidi isogee hadi tarehe 4/8 ambapo ndio itakuwa kilele na ile ya SPORTPESA SIMBA DAY nayo imebidi irudi nyuma kutokana na ratiba ya kuanza michuano ya klabu bingwa barani Afrika na badala ya kilele kuwa tarehe 8/8 sasa itarudi kwa siku mbili na kuwa tarehe 6/8.
Nia na madhumuni ya matukio yote mawili ni kujaribu kutoa nafasi wa wanachama na mashabiki wa timu hizi kuweza kuwatajuwa wachezaji wao,kutambulisha jezi na kutoa burudani,ingawa Yanga wamekwenda mbali zaid katika siku hii kwani wameendelea kufanya shughuliza kijamii maeneo mbalimbali nchi nzima na kutoa misaada kwa wahitaji lakini pia kutoa nafasi kwa mashabiki kukutana katika maeneo yao na kujadili mambo mbalimbali nilipata bahati ya kuhudhuria baadi ya matamasha yanayoendelea nchini ni jambo la fahari sana kwani moyo walionao wapenzi wa timu na kujitoa kwao kama kukitafsiriwa katika uwanja wa kiuchumi na kukuza pato la klabu ni zaidi ya uwekezaji kwani ni hari na morali ya hali ya juu sana.
Kwanini leo nimeona nizingumzie hili,sababu kubwa ni hizi najua Simba na Yanga hakuna ambaye anakubali kusifia au kuona anafanya jambo la mwingine hata kama ni la tija kitu ambacho nadhani si sawa ifike mahali timu zote mbili ziwe flexible katika kuchukuwa yale mazuri ya upende mmoja na kuyaamishia kwao ukizingatia ili maendelea yafikiwe ni lazima ukubali kujifunza bila kujali unajifunza kwa nani kikubwa ni umuhimu wa kile unachojifunza.
Watanzania zaidi ya milioni 40 ni washabiki wa timu hizi mbili ambao kama utaamua kuwashirikisha na kufanya wawe sehemu za hizi timu bila shaka ni faida kubwa itapatikana kwani endapo watawekewa utaratibu wa kusajiliwa kwa njia za kisasa na kutambulika kwa kupewa kadi kulingana na kipata wanachochangia kupitia matawi yao ni zaidi ya makusanyo ambayo yatapatikana uku yakienda kufanya vitu ambayo vitageuka kuwa vitega uchumi kwa klabu hizi kongwe hapa nchini..
Lakini pia endapo Simba na Yanga wataamua kufungua vituo katika kanda mbalimbali na hivi vituo kuwa vinaendesha mafunzo ya soka,kutoa huduma za jamii kama hospitali,shule na vingine vingi hii itapelekea wale mashabiki kuona wanafaidika moja kwa moja na michango yao iwe kwa njia ya malipo ya kadi au namna yeyote itakayopendekezwa na klabu.
Kwani tunajua makao makuu ya hizi timu yapo Dar-es- salaam lakini zina mashabiki nchi nzima kama tulivyoona kwenye wiki ya mwanachi lakini pia hata timu zinapokwenda kucheza mikoani tunaona mwitikio wake.
Jambo lingine umefika wakati wa kufanya jitihada za kujua takwimu halisi za mashabiki ili iwe rahisi kubuni mbinu nzuri na rahisi za kuwafanya wawe sehemu ya timu tofauti na sasa ambapo ni makisio kitu ambacho hakiwezi kuzipeleka timu hizi kwenye mipango na maendeleo ya kweli kwani takwimu ndio dira pekee ya kuelekea kwenye maendeleo na kujua vipaumbele gani vianze na vipi vifuatie,leo hii makampuni ya mawasiliano Tanzania yamefanikiwa sana kukuwa kiuchumi kwa kutumia uwingi wa Watanzania ambapo Watanzania hao sehemu kubwa ni Simba na Yanga,je vilabu vina maono gani na uwingi huu wa watanzania?
Nirudi kwa viongozi tambueni kuwa sio lazima mipango yote ya maendeleo mtakayo ianzisha au kushauriwa ni lazima izae matunda mkiwa bado madarakani ili mpate sifa hapana,mingine acha iende kutoa tija miaka ya baadae na ile hofu ya kuona hamtakuwa sehemu ya mafanikio haina mashiko kwani bado mtabaki kua ni waasisi wa hayo maamuzi na mipango na bado mtakumbukwa tu. Kwani kumekuwa na kasumba ya kutaka vitu vya mda mfupi ili watu waone ninyi ndio mmefanya.
Pia kuna swala la sare au jezi ambazo zimekuwa ndio alama ya timu hizi na vifaa vingine,ifike wakati msimamie kidete kwa kuweka mipango madhubuti kwa kushirikiana na wawekezaji au makampuni mengine ili jezi na vifaa vingine viweze kutoa tija kwa vilabu hivi pendwa ambavyo vina historia kubwa katika Taifa letu.
Mwisho nipende kuwaasa mashabiki na wanachama kuwa tambueni kua hizi ni timu zenu na mafanikio ya timu hizi ndio furaha yenu lazima muwe wepesi katika kusapoti yale ambayo mnaletewa na viongozi wenu ili timu ziweze kusonga mbele msiwe sehemu ya migogoro isiyo na tija na nategemee mtatoa mwitikio chanya kwenye matukio haya makubwa kwa maana ya siku ya kilele cha WIKI YA MWANANCHI na SPORTPESA SIMBA DAY.
natamani kuona watu kutoka mikoa yote mkiujaza uwenja wa Taifa kwa rangi zenu kama ilivyo desturi huku mkiwa watulivu na wasikivu na kuhakikisha amani na upendo wetu Watanzania unatawala na kutamalaki pia.
Timizeni wajibu wenu ili mrudishe mzigo wa lawama kwa viongozi endapo watashindwa kuyatimiza yale mliowatuma.
(Dominick Salamba ni mchambuzi wa michezo, pia anapatikana kupitia Instagram akaunti kupitia @dominicksalamba namba +255713942770)

0 comments:
Post a Comment