KINDA wa umri wa miaka 16, winga wa Guinea-Bissau, Anssumane 'Ansu' Fati akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kusawazisha dakika ya 51 akitokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya or Nelson Semedo katika sare ya 2-2 na wenyeji, Osasuna Uwanja wa El Sadar. Mabao yote ya Osasuna yamefungwa na Roberto Torres dakika ya saba na 81 kwa penalti, wakati bao lingine la Barcelona limefungwa na Arthur dakika ya
64. Winga huyo wa Guinea-Bissau, Fati mwenye umri wa miaka 16 na siku 304, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu mdogo kufunga bao kwenye historia ya miaka 90 ya La Liga baada ya Fabrice Olinga aliyeifungia Malaga akiwa na miaka 16 na siku 98 na Iker Muniain aliyekuwa na miaka 16 na siku 289 alipoichezea kwa mara ya kwanza Athletic Bilbao PICHA ZAIDI GONGA HAPA

0 comments:
Post a Comment