Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba imeendelea kujiimarisha baada ya kusajili wachezaji watano wapya kutoka timu mbalimbali kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Hao ni Yussuph Mhilu kutoka Yanga SC aliyecheza kwa mkopo Ndanda FC msimu uliopita, Zawadi Mauya kutoka Lipuli FC, Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar, Abdallah Seseme kutoka Mwadui FC, Awesu Ally Awesu kutoka Singida United.
Watano hao wanaungana na wengine watatu waliosajiliwa awali, beki Erick Kyaruzi ‘Mopa’ na washambuliaji Frank Ikobela, wote kutoka Mbeya City ya Mbeya na Evarist Mjwahuki kutoka Mbao FC ya Mwanza.
Yussuf Mhilu akikabidhiwa jezi ya Kagera Sugar baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo
Kagera Sugar na Mwadui FC zilinusurika kushuka daraja baada ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupitia mechi zao Play-Off dhidi ya Pamba SC na Geita Gold Mine za Daraja la Kwanza.
Mabao ya Ally Ramadhani dakika ya 51 na Japhet Makalayi dakika ya 59 yaliipa Kagera Sugar ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba SC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Juni 9 baada ya timu hizo kutoka sare ya kwenye mchezo wa kwanza Juni 3 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Na hiyo ni baada ya Kagera Sugar kumaliza nafasi ya 18 katika Ligi Kuu, nyuma ya Mwadui FC iliyomaliza nafasi ya 17 ambayo iliitoa Geita Gold katika mechi ya mchujo.

0 comments:
Post a Comment