Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba imeendelea kujiimarisha baada ya kumsajili kipa Benedicto Tinocco kutoka kwa ndugu zao, Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Taarifa ya Kagera Sugar kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba kipa huyo wa zamani wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam amekamilisha uhamisho wake kutoka Manungu.
Kutua kwa Tinocco ambaye amewahi kuwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kunafanya idadi ya jumla ya wachezaji 11 wapya kusajiliwa, wakiwemo wawili wa kigeni, Mganda Jackson Kibirige kutoka Bakavu Dawa FC ya Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo (DRC) na Moussa Hadji Mosi kutoka Leslierres ya Ligi Kuu ya kwao, Burundi.
Benedicto Tinocco ametua Kagera Sugar ya Bukoba kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro
Wengine wote ni wazawa Abdul Swamadu Kassim kutoka Malindi FC ya Zanzibar, Yussuph Mhilu kutoka Yanga SC aliyecheza kwa mkopo Ndanda FC msimu uliopita, Zawadi Mauya kutoka Lipuli FC, Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar, Abdallah Seseme kutoka Mwadui FC, Awesu Ally Awesu kutoka Singida United, Erick Kyaruzi, Frank Ikobela, wote kutoka Mbeya City ya Mbeya na Evarist Mjwahuki kutoka Mbao FC ya Mwanza.
Kagera Sugar imepania kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao baada ya kunusurika kushuka Daraja msimu uliopita.
Ikumbukwe Kagera Sugar na Mwadui FC zilinusurika kushuka daraja baada ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupitia mechi zao Play-Off dhidi ya Pamba SC na Geita Gold Mine za Daraja la Kwanza.
Mabao ya Ally Ramadhani dakika ya 51 na Japhet Makalayi dakika ya 59 yaliipa Kagera Sugar ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba SC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Juni 9 baada ya timu hizo kutoka sare ya kwenye mchezo wa kwanza Juni 3 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Na hiyo ni baada ya Kagera Sugar kumaliza nafasi ya 18 katika Ligi Kuu, nyuma ya Mwadui FC iliyomaliza nafasi ya 17 ambayo iliitoa Geita Gold katika mechi ya mchujo.

0 comments:
Post a Comment