Na Mwandishi Wetu, DAR ES SASLAAM
KLABU ya Difaa Hassan El-Jadidi msimu ujao itakuwa na wachezaji wawili wa Kitanzania, ambao ni beki Nickson Clement Kibabage na kiungo mshambuliaji, Simon Happygod Msuva.
Baada ya kuonja matunda ya Msuva kwa misimu miwili tangu imsajili kutoka kwa vigogo wa Tanzania, Yanga SC msimu huu Jadida imesajili beki, Kibabage kutoka Mtibwa Sugar.
Kibabage ni mmoja wa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Beki chipukizi, Nickson Clement Kibabage (kushoto) akiwa na kiungo Mtanzania mwenzake, Simon Muva mazoezini na klabu ya Difaa Hassan El-Jadidi nchini Morocco
27 na 99; Hao ni wachezaji wa Kitanzania wakiwa na wenzao Difaa Hassan El-Jadidi
Na baada ya hapo klabu ya Mtibwa Sugar ikampeleka kwa mkopo Njombe Mji ili kupata uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Msimu uliopita akarejea Manungu kuendelea kuchezea kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 na mara chache akipewa nafasi cha kwanza.
Akaiongoza Mtibwa Sugar kutwaa ubingwa wa U20 wa Ligi ya Taifa mwezi uliopita mjini Dar es Salaam kwa ushindi wa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0.
Tayari Kibabage ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes ambaye bila shaka muda si mrefu atapandishwa kikosi cha wakubwa.

0 comments:
Post a Comment