Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Yanga upo katika mchakato wa kutafuta Mkurugenzi wa Ufundi na Maafisa wengine wa Sekretarieti katika kuimarisha mfumo wake wa utawala uliolega kwa sasa.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela amesema kwamba wametoa tangazo la nafasi za kazi kwenye vyombo vya Habari kupata watu wanaowahitaji.
Mwakalebela, Katibu wa zamani wa Shirikisho la SOka Tanzania (TFF) chini ya Rais, Leodegar Tenga amewataja wanaohitajika pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi, wengine ni Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Mashindanona Mkurugenzi wa Masoko, Matukio na Brandi.
Mwakalebela aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Mtibwa Sugar ikichukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mara mbili mfululizo 1999 na 2000 amewataja wengine ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala na Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama.
Yanga SC ipo chini ya uongozi mpya chini ya Mwenyekiti, Dk. Mshindo Mbette Msolla, Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars waliochaguliwa Mei 5, mwaka huu katika uchaguzi uliofanyika Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Osyterbay mjini Dar es Salaam.
Siku hiyo, Msolla alipata jumla ya kura 1,276 dhidi ya 60 tu za Daktari mwenzake, Jonas Benedict Tiboroha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo chini ya uongozi uliopita.
Mwakalebela alipata kura 1,206 akiwashinda Janneth Mbene (Mbunge)aliyepata kura 61, Titus Osoro kura 17, Yono Kevela kura 31 na Chota Chota kura 12.
Walioshinda nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Islam aliyepata 1,206, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba kura 1,174, Dominick Ikute kura 1,088, Kamugisha Kalokola kura 1,072, Arafat Haji kura 1,024, Salum Ruvila kura 976, Saad Khimji kura 788 na Rodgers Gumbo kura 776.
Uchaguzi huo ulifuatia kujiuzulu kwa viongozi wote waliongia madarakani Juni 11 mwaka 2016, Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wao, Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay, Hussein Nyika, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Inspekta Hashim Abdallah.
Pamoja na kuwa kocha wa Taifa Stars, Dk. Msolla pia amewahi kuwa mtumishi wa Serikali kwa nafasi mbalimbali, ikiwemo Ukurugenzi wa Uendelezaji wa Mazao katika Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakati wa awamu ya Nne chini ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

0 comments:
Post a Comment