Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Kigoma imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza wa taifa ya vijana chini ya umri wa miaka (U15) baada ya kuichapa Mjini Magharibi bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Bao pekee lililoipa ushindi Kigoma lilifungwa na mshambuliaji wake hodari, Hemed Hamisi dakika ya 35 akitumia makosa ya beki wa Mjini Magharibi, Abdulrazak Vuai Mohamed aliyepiga fyongo katika jitihada za kuokoa na mpira ukamkuta mfungajii.
Jumla ya timu 34 kutoka mikoa yote ya Tanzania zilishiriki michuano hiyo na Kigoma ambao kiasili ni mkoa wenye historia ya kutoa vipaji vingi imedhihirisha ubora wake kwa mara nyingine.

0 comments:
Post a Comment