Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BEKI anayecheza nafasi zote za ulinzi na kiungo, Shomari Kapombe jana aliumia mazoezini kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Uwanja wa Taifa Dar es Salaam inayojiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zikazofanyika baadaye mwezi huu nchini Misri.
Kapombe, beki wa Simba SC ni miongoni mwa wachezaji 39 walioitwa kwenye kikosi cha awali cha Taifa Stars kilichoingia kambini juzi hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam kwa maandalizi ya awali ya AFCON kabla ya kikosi kwenda Alexandria Juni 7.
Kapombe ameitwa Taifa Stars akitoka kuwa nje kwa zaidi ya miezi saba akiuguza majareha aliyoyapata mwezi Novemba mwaka jana nchini Afrika Kusini alipokuwa mazoezini pia na kikosi cha timu ya taifa kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho.
Pole; Shomari Kapombe yuko hatarini kuzikosa Fainali za AFCON baada ya kuumia mazoezini Taifa Stars
Kocha Emmanuel Amunike aliamua kumjumuisha katika kikosi hicho cha awali kilichotangaza mwezi Mei mwaka huu, baada ya mchezaji huyo kupona majeraha yake na kuanza mazoezi tayari kwa kurudi dimbani licha ya klabu yake ya Simba kutomtumia katika mechi za mwisho za Ligi Kuu Tanzania Bara.Leo Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo amethibitisha kuwa mchezaji huyo amejitonesha majeraha hayo wakati akiendelea na mazoezi katika kambi ya Taifa Stars iliyoanza rasmi Juni 01, 2019 kwenye Hoteli ya White Sands hivyo kwa sasa anasubiri hatma yake kwenye kikosi cha mwisho kitakachotajwa hivi karibuni.
“Shomari Kapombe amejitonesha wakati akiendelea na programu ya timu ya taifa hivyo kwasasa hayuko na wenzake lakini anaendelea kufuatilia programu ya mazoezi mpaka hapo mwalimu atakapotaja kikosi cha mwisho”, amesema Ndimbo.
Taifa Stars itaondoka na wachezaji 32 kwenda kambini mjini Alexandria, Misri baada ya kuchujwa saba na kati ya hao ni 23 tu watashiriki AFCON.
Wachezaji wengine wataendelea kubaki kambini kwa maandalizi ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Kikosi cha kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kitaanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wa AFCON, Misri Juni 13, mwaka huu Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Baada ya hapo Taifa Stars itacheza mechi zake tatu za Kundi C mfululizo ikianza na Senegal Juni 23, Kenya Juni 27 na kumaliza na Algeria Julai 1 kuangalia matokeo yake kama yataipeleka hatua ya mtoano.

0 comments:
Post a Comment