// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BENO KAKOLANYA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA SIMBA SC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BENO KAKOLANYA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA SIMBA SC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 14, 2019

    BENO KAKOLANYA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA SIMBA SC

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA kipa wa Yanga SC, Beno Kakolanya akisaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mahasimu, Simba SC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
    Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba wamekwishamalizana na Kakolanya baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuwa mlinda mlango mpya wa klabu hiyo.
    “Hakuna ubishi kuwa huyu ni moja ya makipa wenye uwezo mkubwa nchini na tunaamini akishirikiana na wenzake katika kikosi chetu watatuwezesha kuongeza ukubwa wa timu na kutupatia mataji msimu ujao,”imesema taarifa ya Simba SC. Tumeshamalizana nae kwa mkataba wa miaka miwili.

    Kusajiliwa kwa Kakolanya kunafanya idadi ya jumla ya makipa wanne Simba SC, Aishi Manula, Deogratias Munishi ‘Dida’ na chipukizi Abdul Salim anayeinukia vizuri.
    Kakolanya alisajiliwa Yanga SC mwaka juzi kwa ajili ya kwenda kuchukua nafasi za makipa walioonekana wanaelekea kuchoka, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, lakini hata hivyo akashindwa pamoja na wawili hao kuondoka.
    Kwa misimu miwili aliyokaa Yanga, David Kakolanya amedaka mechi 24 tu, kabla ya kujiondoa mwenyewe akiituhumu klabu kukiuka vipengele vya mkataba ambao mwishowe ulivunjwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENO KAKOLANYA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top