Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI mpya wa Blackpool FC ya Daraja la Pili England, Adi Yussuf ni miongoni mwa wachezaji walioripoti katika kambi ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam katika siku ya kwanza leo kwa maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baadaye mwezi huu nchini Misri.
Adi Yussuf aliyejiunga na Blackpool akitokea Solihull Moors ya Daraja la Sita kama mchezaji huru ameripoti leo Whites Sands na kufanyiwa vipimo vya afya.
Meneja wa Taifa Stars, Danny Msangi amesema kwamba ni mchezaji mmoja tu, kiungo Himid Mao ambaye hajaripoti kwa sababu atakuwa anaichezea klabu yake, Petrojet FC mchezo wa mwisho wa msimu wa Ligi Kuu ya Misri Jumatatu dhidi ya Al Mokawloon ikihitaji ushindi ili kuepuka kushuka daraja.
Wachezaji 38 wameingia kambini leo Taifa Stars hoteli ya White Sands hadi Juni 7 kwa maandalizi ya awali ya AFCON kabla ya kikosi kwenda Alexandria.
Kikosi kitaondoka na wachezaji 32 baada ya kuchujwa saba kutoka 39 walioitwa akiwemo Mao na kati ya hao ni 23 tu watashiriki AFCON.
Wachezaji wengine wataendelea kubaki kambini kwa maandalizi ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Kikosi cha kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kitaanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wa AFCON, Misri Juni 13, mwaka huu Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Baada ya hapo Taifa Stars itacheza mechi zake tatu za Kundi C mfululizo ikianza na Senegal Juni 23, Kenya Juni 27 na kumaliza na Algeria Julai 1 kuangalia matokeo yake kama yataipeleka hatua ya mtoano.
Kikosi kilichoingia kambini leo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC), Suleiman Salula (Malindi SC) na Aaron Lulambo (Tanzania Prisons).
Mabeki; Claryo Boniface (U20), Hassan Kessu (Nkana FC, Zambia), Vincent Philipo (Mbao FC), Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni (Simba SC), Kelvin Yondan, Gardiel Michael (Yanga SC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Ally Ally (KMC) na Kennedy Wilson (Singida United).
Viungo ni Feisal Salum, Ibrahim Ajibu (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba SC), Shiza Kichuya (ENNPI, Misri), Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi Morocco) na Farid Mussa (Tenerife, Hispania).
Washambuliaji ni Yahya Zayd (Ismailia, Misri), Shaaban Iddi Chilunda (Tenerife, Hispania), Rashid Mandawa (BDF, Botswana), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Khamis (Kagera Sugar), Kelvin John (Serengeti Boys), Adi Yussuf (Solihull Moors, England), John Bocco (Simba SC), Thomas Ulimwengu (JS Saoura, ALgeria) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).
Wachezaji wengine beki Ally Mtoni, kiungo Freddy Tangalu wa Lipuli FC na mshambuliaji Miraj Athumani ‘Madenge’ wa Lipuli FC, mabeki David Mwantika, Aggrey Morris, viungo Frank Domayo na Mudathir Yahya wa Azam FC watajiunga na wenzao kesho baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mbali na Taifa Stars kupangwa Kundi C AFCON 2019 pamoja na jirani zao, Kenya, Algeria na Senegal – wenyeji, Misri wapo Kundi A pamoja na na Zimbabwe, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kundi B linaundwa na Burundi, Madagascar, Guinea na Nigeria, Kundi D linaundwa na Namibia, Afrika Kusini, Ivory Coast na Morocco, wakati Kundi E kuna Angola, Mauritania, Mali na Tunisia na Kundi F ni Guinea Bessau, Benin, Ghana na mabingwa watetezi, Cameroon.
Taifa Stars imefuzu AFCON ya mwaka huu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi L kwa pointi zake nane, nyuma ya jirani zao wa Afrika Mashariki, Uganda walioongoza kwa pointi zao 13 wakizipiku Lesotho iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.
Mwaka huu, Tanzania itashiriki AFCON kwa mara ya pili tu kihistoria baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria ambako ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji, Nigeria, Misri na Ivory Coast na kushika mkia.
Mwaka 1980 ilifungwa mechi mbili, 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast na kuishia Raundi ya kwanza tu, wakati timu nane tu zinashiriki michuano hiyo.
Michuano itaanza Juni 21 hadi Julai 19 na Taifa Stars itachezea mechi zake Uwanja wa Juni 30 na Al Salam mjini Cairo.
Na katika CHAN, Taifa Stars itaanzia nyumbani dhidi ya Sudan Julai 26 kabla ya kurudiana Agosti 2 na ikifuzu mtihani huo itamenyana na mshindi kati ya Kenya na Burundi.

0 comments:
Post a Comment