// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KAGERA SUGAR KUMENYANA NA PAMBA, MWADUI FC NA GEITA GOLD KATIKA ‘PLAY-OFFS’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KAGERA SUGAR KUMENYANA NA PAMBA, MWADUI FC NA GEITA GOLD KATIKA ‘PLAY-OFFS’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, May 29, 2019

    KAGERA SUGAR KUMENYANA NA PAMBA, MWADUI FC NA GEITA GOLD KATIKA ‘PLAY-OFFS’

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BODI ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) imetoa ufafanuzi kuhusu nafasi zinapopaswa kukaa timu za Stand United na Kagera Sugar kwenye msimamo wa ligi kuu 2018/19 baada ya mechi za mwisho kuhitimishwa jana.
    Akizungumza na wanahabari leo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema timu inayostahili kukaa nafasi ya 19 na kushuka daraja moja kwa moja ni Stand United huku Kagera Sugar ikistahili kukaa nafasi ya 18.
    Wambura amesema licha ya timu hizo kulingana pointi, kwa timu zote kuwa na pointi 44, Kagera Sugar ina faida ya kuwa na tofauti kubwa ya magoli ya kufunga na kufungwa ambayo ni -10 wakati Stand United ina tofauti ndogo ya magoli ya kufunga na kufungwa ambayo ni -12.

    Kwa ufafanuzi huo, Kagera Sugar na Mwadui FC sasa watalazimika kupitia kwenye hatua ya mtoano (Play-Off) dhidi ya timu zilizotoka daraja la kwanza ili kujinusuru na janga la kushuka daraja wakati Stand United ikiungana na African Lyon kushuka daraja moja kwa moja.
    Mechi za kwanza za mtoano zitapigwa Juni 2, Kagera ikianzia ugenini Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na Mwadui ikianzia ugenini dhidi ya Geita kabla ya marudiano Juni 8 Uwanja wa Kaitaba Bukoba na Mwadui Complex, Shinyanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR KUMENYANA NA PAMBA, MWADUI FC NA GEITA GOLD KATIKA ‘PLAY-OFFS’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top