Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO kati ya Azam FC na Yanga SC utafanyika Uwanja Uhuru badala ya Taifa mjini Dar es Salaam Aprili 29 kuanzia Saa 10:00 jioni.
Azam FC watakuwa wenyeji wa Yanga SC Jumatatu ijayo Uwanja Uhuru katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Na kwa mujibu wa barua iliyotumwa na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), mabadiliko hayo yanatokana na ukarabati utakaofanywa Uwanja wa Taifa baada ya kumalizika kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 Jumapili wiki hii.
Azam FC imeanza mazoezi ikiwa na kikosi kamili, ambapo kwa mujibu wa programu kikosi hicho kinatarajia kujifua kwa siku sita hadi kuelekea mtanange huo, ambao utakuwa ni wa kwanza kwa timu zote kukutana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu huu.
Kikosi hicho ndani ya siku hizo sita za mazoezi, kitajifua mara moja kila siku jioni, isipokuwa keshokutwa Alhamisi kikitarajia kufanya mara mbili asubuhi na jioni huku Ijumaa hii kikitarajia kucheza mchezo wa kujiweka sawa dhidi ya timu ya vijana ya Azam FC.
Yanga SC nao wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini mjini Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment