Luis Suarez akiwa amemkumbatia mchezaji wa Villarreal, Santi Cazorla baada ya Nyota wa Uruguay kuifungia Barcelona bao la kusawazisha dakika ya 90 na ushei ikitoa sare ya 4-4 na wenyeji wao hao katika mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Ceramica mjini Villarreal. Mabao mengine ya Barcelona yalifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 12, Malcom dakika ya 16 na Lionel Messi dakika ya 90, wakati ya Villarreal yalifungwa na Samuel Chimerenka Chukwueze dakika ya 23, Karl Brillant Toko Ekambi dakika ya 50, Vicente Iborrasakika dakika ya 62 na Carlos Arturo Bacca dakika ya 80. Barcelona inafikisha pointi 70 baada ya sare hiyo katika mechi ya 30 na inaendelea kuongoza La Liga kwa pointi nane zaidi yaa Atletico Madrid wanaofuatia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Eric Alagidede opens up on fallout with Nsoatreman FC, cites political
tensions
-
Former General Manager of Nsoatreman FC Eric Alagidede has opened up about
the fallout with his former club, revealing that political tensions were at
the ...
34 minutes ago
0 comments:
Post a Comment