TIMU ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imetanguliza mguu mmoja Nusu Fainali ya Ligi Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri leo Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe mjini Pretoria.
Sasa Mamelodi Sundowns inayofundishwa na kocha mzalendo, Pitso John Mosimane itakuwa na kazi nyepesi ya kuulinda ushindi wake mnene kwenye mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Aprili 13 mjini Alexandria.
Mabao ya Mamelodi leo yamefungwa na Themba Zwane dakika ya 14, Wayne Arendse dakika ya 24, Ricardo Nascimento kwa penalti dakika ya 47, Leandro Gastón Sirino dakika ya 62 na Phakamani Mahlambi dakika ya 83.
Mechi za kwanza za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo, Simba SC imelazimishwa sare ya 0-0 na Tout Puissant Mazembe Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Simba SC watajilaumu wenyewe kwa sare hiyo ya nyumbani, kwani walipoteza nafasi nzuri mno ya kuibuka na ushindi kipindi cha pili, kufuatia Nahodha wake, John Raphael Bocco kukosa penalti.
Mchezo kati ya Horoya ya Guinea na Wydad Casablanca unaendelea hivi sasa na baadaye CS Constantine ya Algeria itamenyana na Esperance Uwanja kuanzia Saa 4:00 usiku.

0 comments:
Post a Comment