// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAMADHANI KABWILI AITWA KIKOSI CHA NGORONGORO HEROES MECHI NA ERITREA MACHI 31 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAMADHANI KABWILI AITWA KIKOSI CHA NGORONGORO HEROES MECHI NA ERITREA MACHI 31 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 15, 2019

    RAMADHANI KABWILI AITWA KIKOSI CHA NGORONGORO HEROES MECHI NA ERITREA MACHI 31

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetaja kikosi cha wachezaji 24 wa kuunda timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes kiitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Eritrea, Machi 31, mwaka huu.
    Wachezaji walioteuliwa kuunda kikosi hicho ni makipa Ramadhani Kabwil wa Yanga SC, Ali Salim wa Simba SC na Zubeiry Masoud wa shule ya sekondari ya Makongo, Dar es Salaam. 
    Mabeki ni Israel Mwenda, Hans Msonga wote wa Alliance FC ya Mwanza, Nickson Kibabage, Dickson Job wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Ali Msengi wa KMC FC ya Dar es Salaam, Mohamed Rashid wa Singida United na Henrick Nkosi wa Ndanda FC ya Mtwara. 

    Viungo ni Mohamed Mussa, Akram Munir, Issa Abushehe, Hamisi Kanduru wa Coastal Union ya Tanga, Rashid Juma wa Simba SC, Jafari Mtoo wa Arusha Academy, Abubakar Juma wa Mtibwa Sugar, Najib Mohamed na Assad Juma wa Singida United. 
    Washambuliaji ni Muhsin Makame wa Coastal Union, Habibu Kyombo wa Singida United, Said Mussa wa African Lyon, Nashon Naftari wa JKT Tanzania na Kelvin Sospeter wa KMC FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAMADHANI KABWILI AITWA KIKOSI CHA NGORONGORO HEROES MECHI NA ERITREA MACHI 31 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top