• HABARI MPYA

        Tuesday, February 12, 2019

        SIMBA ILIVYONDELEZA UBABE WAKE KWA WAARABU DAR

        Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akiwatoka mabeki wa Al Ahly katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Simba SC imeshinda 1-0, bao pekee la Kagere dakika ya 65 na kuendeleza rekodi yake ya kuzifunga timu za Kaskazini mwa Afrika nyumbani   
        Meddie Kagere, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda akitafuta maarifa ya ya kuwatoka wachezaji wa Al Ahly 
        Mshambuliaji Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi akitafuta mbinu za kumpita Karim Nedved wa Al Ahly 
        Emmanuel Okwi akijivuta kupiga shuti pembeni ya Ali Maaloul
        Kiungo Mzambia wa Simba, Clatous Chama (kushoto) akimpiga chenga Ramadan Sobhi wa Al Ahly
        Beki wa Simba Zana Coulibally kutoka Burkina Faso (kushoto) akijaribu kuzuia mpira unaopigwa na Ali Maaloul
        Clatous Chama akipambana katikati ya wachezaji wa Zamalek
        Mwenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi ya Simba, Mohammed 'Mo' Dewji akishangilia bao la Kagere leo
        Kikosi cha Simba SC kilichoanza kwenye mechi dhidi ya Al Ahly leo
        Kikosi cha Al Ahly kilichochapwa 1-0 na Simba leo Uwanja wa Taifa
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: SIMBA ILIVYONDELEZA UBABE WAKE KWA WAARABU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry